WAZAZI WATAKIWA KUTEKELEZA JUKUMU LA KUDUMISHA NIDHAMU MIONGONI MWA WANAO.
Wito umetolewa kwa wazazi katika kaunti hii ya Pokot magaribi kushirikianba na walimu katika kuhakikisha nidhamu miongoni kwa wanafunzi.
Naibu mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Chepkono Jodina Wekesa amesema wengi wa wanafunzi wa kiume wanasusia masomo na kujihusisha na biashara ya boda boda kutokana na hali kuwa wengi wao wanaishi katika nyumba za kupanga, na hivyo kujihusisha na maswala mengine mengi bila ya ufahamu wa wazazi na uongozi wa shule.
Bi Wekesa amesema ni jukumu la mzazi kufuatilia mienendo ya wanao hasa wale ambao wanaishi katika nyumba za kupanga, ikiwemo kuwazuru maeneo wanakoishi pamoja na kufuatilia jinsi wanavyoendelea na masomo shuleni, na kutowaachia walimu jukumu hilo.
Kuhusu swala la mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi wa kike, Bi Wekesa amesema kuwa visa hivi vimepungua pakubwa mwaka huu ikilinganishwa na ilivyoshuhudiwa mwaka jana hali anayosema ilichangiwa pakubwa na likizo ndefu iliyosababishwa na janga la corona.