WAZAZI WATAKIWA KUSHUGHULIKIA NIDHAMU YA WANAO.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya upili ya chewoyet katika kaunti hii ya pokot magharibi Ruth Kisabit ameshutumu maandamano yaliyoandaliwa na baadhi ya wakazi wa mjini makutano kukashifu uongozi wa shule hiyo kwa madai ya kuwatuma nyumbani wanafunzi nyakati za jioni.
Kisabit ambaye pia ni waziri wa fedha katika serikali ya kaunti hii ya pokot magharibi amekashifu maandamano hayo yaliyoelekezwa hadi shuleni humo akiwataka wananchi kufuata taratibi zinazostahili katika kuwasilisha malalamishi yao iwapo kuna jambo wasiloridhika nalo.
Aidha kisabit amewahimiza wazazi kufuatilia mienendo ya wanao na kuchangia pakubwa katika swala la nidhamu kwa na kutowaachia walimu pekee iwapo wanahitaji matokeo bora kutoka kwa wanao huku pia akiwahimiza kuhakikisha wanahudhuria masomo kila mara.
Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo kiminisi Bararasa amewataka wazazi kushirikiana na shule hiyo kwa kulipa karo kwa wakati ili kuywaweazesha wanao kusalia shuleni, huku akitoa wito kwa viongozi wa kisiasa kutoingiza siasa katika shule.