WAZAZI WATAKIWA KULIPA KARO YA WANAO


Baadhi ya wakuu wa shule katika kaunti hii ya pokot magharibi wametoa wito kwa wazazi kujikakamua na kulipa karo ya wanao ili kuwezesha kuendeshwa shughuli muhimu katika shule hizo licha ya hali ngumu ya kiuchumi inayoshuhudiwa sasa.
Wakiongozwa na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wavulana ya Karenger Simon mutambo, wakuu hao wamesema shule hizo zimezingatia agizo la wizara ya elimu kupunguza karo na wazazi wanafaa pia kutekeleza sehemu yao licha ya serikali ya kaunti pia kulipa sehemu ya karo kupitia fedha za basari.
Wakati uo huo Mutambo amewataka wazazi kutokuwa na hofu kuhusu usalama wa wanao wanapokuwa shuleni kwani mikakati madhubuti imewekwa kuhakikisha kuwa hakutakuwa na kisa chochote cha maambukizi ya corona kitakachoripotiwa miongoni mwa wanafunzi.