WAZAZI WATAKIWA KUFANYA JUHUDI ZAIDI KUMSHUGHULIKIA MTOTO WA KIAFRIKA.


Ni wakati wazazi katika kaunti hii ya pokot magharibi wanastahili kuamka na kujiunga na maeneo mengine pamoja na mataifa ya bara zima la afrika katika kuchangia juhudi za kuhakikisha mtoto wa kiafrika anashughulikiwa inavyostahili.
Akizungumza eneo la sigor katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kiafrika, mwenyekiti wa mtandao wa kuwalinda watoto child protection network ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya st. Elizabeth murpus Carolyne Menach, amesema kuwa idadi kubwa ya watoto kaunti hii wametelekezwa na wazazi hali ambayo imewanyima haki zao za kimsingi.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na maafisa katika shirika la world vision Teresa Cheptoo pamoja na Mercy Cheruto ambao pia wamesema jamii ina jukumu kubwa la kufanya katika kuokoa watoto hasa wa kike kutoka tamaduni kama vile ukeketaji na ndoa za mapema ili kuwapa fursa ya kupata elimu.
Kwa upande wake naibu kamishina eneo la pokot ya kati Naphtali korir amesema serikali kwa ushirikiano na wadau mbali mbali wameendelea kuweka mikakati kuhakikisha kuwa mtoto wa kiafrika hasa mkenya anapata haki kulingana na sheria za nchi.