WAZAZI WASIOWAPELEKA WANAO SHULENI WAONYWA.


Wazazi eneo la pokot ya kati katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanao wanahudhuria masomo wakati huu ambapo shule zimefunguliwa kwa muhula wa kwanza huku waliofanya mtihani wa KCPE wakijiunga na kidato cha kwanza.
Ni wito wake naibu kamishina wa eneo la pokot ya kati Were Simiyu ambaye amesema kuwa elimu ni bure na ni lazima kwa kila mtoto huku akiwaagiza machifu kuhakikisha watoto waliotimu umri wa kwenda shule wanahudhuria masomo.
Akizungumza na kituo hiki simiyu aidha ameonya kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mzazi ambaye atakosa kumpeleka shule mwanaye aliyetimu umri wa kwenda shule, pamoja na chifu wa eneo husika.