WAZAZI WASHAURIWA KUWAVUSHA WANAO MITO WANAPOENDA SHULENI
Wito umetolewa kwa wazazi eneo la Kongelai kaunti hii ya Pokot Magharibi kuwa makini na wanao hasa msimu huu wa mvua kubwa na kuhakikisha wanawavusha mito ambayo huenda imefurika ili kuzuia maafa.
Ni wito ambao umetolewa na mzazi mmoja kutoka eneo hilo Nelly Pusha ambaye aidha amewaomba walimu kutowatuma wanafunzi nyumbani kutafuta karo na badala yake kuwapigia wazazi simu ili kuzuia hali ya kunyeshewa na mvua kubwa ambayo inaendelea kushuhudiwa kaunti hii na kisha baadaye kusababisha madhara.
Wakati uo huo amemtaka mwakilishi wadi ya Riwo David alukulem kuhakikisha kisima cha shule ya msingi ya Simotwo kinarekebishwa ili kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kupata maji safi.