WAZAZI WALAUMIWA KWA KUWATELEKEZA WANAO BUNGOMA.


Wazazi katika kaunti ya Bungoma wamelaumiwa kwa kufeli katika majukumu ya kuwatunza na kuwapa ushauri wanao jambo ambalo lilichangia idadi kubwa ya wanafunzi kuufanya mtihani wa kcse mwaka 2020 kaunti hiyo wakiwa wajawazito.
Akizungumza mjini Webuye naibu kamishina wa wilaya ya Webuye magharibi Kipketich Lotyatya amesema wazazi wengi wameachia walimu majukumu ya kuwatunza wanao hivyo kuwafanya wanafunzi wengi kujihusisha na mimba za mapema.
Ikumbukwe kaunti ya Bungoma ilitajwa kuwa na idadi ya juu zaidi ya wanafunzi waliofanya mtihani wa KCSE wakiwa wajawazito.
Wakati uo huo Lotyatya ameonya wazazi dhidi ya kuwapa wanao wenye umri wa kuwa shuleni pikipiki ili kuhudumu katika sekta ya boda boda, hali ambayo imechangia ajali nyingi za barabarani akisema watakaopatikana watachukuliwa hatua kali za sheria.