WAZAZI WALAUMIWA KWA KUKITHIRI MIMBA ZA MAPEMA
Siku chache tu baada ya shirika la AMREF kutoa takwimu zilizoashirika kuwa visa vya mimba za mapema katika kaunti hii ya Pokot magharibi zinazidi viwango vya kitaifa seneta wa kaunti hii Samwel Poghisio amelalamikia kukithiri visa hivyo.
Akizungumza katika mahojiano na kituo hiki, Poghisio amesema kuwa huenda idadi ya juu ya visa hivi imeripotiwa kutokana na utepetevu miongoni mwa wazazi katika kufuatilia mienendo ya wanao hasa wakati walipokuwa nyumbani katika likizo ndefu iliyosababishwa na ujio wa janga la corona.
Wakati uo huo Poghisio amewataka wadau wengine ikiwemo walimu kuhakikisha kuwa wanatia maadili mema miongoni mwa wanafunzi hasa wanapoendeleza shughuli za kuwafunza wakati wanapokuwa shuleni ili kupunguza visa hivi katika kaunti hii ya pokot magharibi.