WAZAZI WALALAMIKIA MTAALA WA UMILISI CBC KWA GHALI.


Chama cha wanasheria LSK kinapotarajiwa kufika mahakamani kupinga utekelezwaji wa mtaala wa elimu CBC, baadhi ya wazazi katika kaunti hii ya pokot magharibi wameendelea kulalamikia mtaala huo ambao wamedai ni ghali mno ikilinganishwa na mtaala wa elimu wa 8.4.4.
Aidha wazazi wamesema kuwa mtaala huo ulianza kutekelezwa bila kutoa elimu kwa wazazi kuuhusu hali ambayo inafanya vigumu kuumudu hasa ikizingatiwa vifaa vingi ambavyo wanahitajika kununua kwa ajili ya matumizi ya wanao shuleni.
Wametaka utekelezwaji wa mtaala huo kusitishwa na kurejeshwa ule wa 8.4.4.
Hata hivyo wapo baadhi ya wazazi ambao wamechangamkia mtaala huo wa umilisi CBC.