WAZAZI WALALAMIKIA GHARAMA YA JUU YA BIDHAA ZA SHULE WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA WAKISAJILIWA.


Usajili wa wanafunzi ambao wanajiunga na kidato cha kwanza ukiendelea kote nchini baada ya shughuli hiyo kung’oa nanga jumatano, wazazi katika kaunti hii ya Pokot Magharibi wakilalamikia kupanda kwa gharama ya maisha.
Wazazi hao wanasema kuwa kupanda kwa bei ya mafuta ni miongoni mwa sababu ambazo zimechangia pakubwa katika kupanda kwa gharama ya maisha huku baadhi wakilaumu baadhi ya wafanyibiashara kutumia fursa hii kupandisha maradufu bei ya bidhaa za shule.
Wazazi hao sasa wameitaka wizara ya elimu kuingilia kati hasa kuhusu swala la ununuzi wa bidhaa za shule ambapo wadai baadhi ya shule zimeshirikiana na wauzaji wa bidhaa hizo kuwadhulumu wazazi kwa kupandisha bei mara dufu.