WAZAZI WAGHADHABISHWA NA KUTUMWA NYUMBANI WANAFUNZI KWA AJILI YA KARO.


Waziri wa elimu prof. George magoha ametakiwa kuingilia kati na kuwakanya wakuu wa shule dhidi ya kuwarejesha nyumbani wanafunzi kwa ajili ya karo.
Baadhi ya wazazi wa kaunti hii ya Pokot magharibi wamesema kuwa baadhi ya shule zimeanza kuwarejesha nyumbani wanafunzi kutafuta karo siku chache tu baada ya kufunguliwa shule kwa muhula wa kwanza.
Aidha wazazi hao wamewataka walimu kuwasiliana nao kuhusu maswala ya karo na kuwaacha wanafunzi kusalia shuleni ikizingatiwa shughuli za masomo zilirejelewa wakati ambapo wazazi wengi walikuwa hawajapata fedha.