WAZAZI POKOT MAGHARIBI WATAKIWA KUIPA KIPAU MBELE ELIMU YA MTOTO WA KIKE

Na Benson Aswani
Wazazi katika kaunti hii ya pokot magharibi wametakiwa kutii agizo lililotolewa na wizara ya elimu nchini na kuhakikisha kuwa wanao hasa wa kike walio na ujauzito wanendelea na masomo yao na kutowalazimishia ndoa za mapema.
Ni wito wake mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wasichana ya our lady of Mercy Adurkoit Mary Stela Watima ambaye amesema kuwa wanafunzi hao wana haki ya kuendela na masomo hadi wakati ambapo wanafaa kujifungua ndipo wataruhusiwa kuondoka shuleni.
Aidha amesema kuwa wanafunzi hao wanastahili kuruhusiwa kurejea shuleni kuendelea na masomo miezi mitatu baada ya kujifungua
Wakati uo huo Watima amesema kuwa shule hiyo ina wanafunzi wengi ambao wanahitaji msaada kuendelea na masomo yao kutokana na hali ya umasikini ya familia zao akitoa wito kwa wadau mbali mbali kujitokeza na kuwafadhili wanafunzi hao kupata mahitaji yao kimasomo.