WAZAZI POKOT MAGHARIBI WATAKA KUANGAZIWA MATUMZI YA FEDHA ZA BASARI.


Wazazi wa wanafunzi waliofanya mtihani wa kitaifa wa KCPE kaunti ya pokot magharibi sasa wanaiomba serikali kuu na ile ya kaunti kuangazia wanafunzi wanaotoka katika jamii sisizojiweza wakati wa kutoa fedha zinazotengwa kuwafadhili wanafunzi hao.
Kulingana na wazazi hawa , fedha za basari zinazofaa kuwafaidi wanafunzi wanaotoka katika jamii maskini mara nyingi huishia kufaidi jamii zinazoweza kujimudu kinyume na matarajio ya wengi.
Ikumbukwe kwamba Kila mwaka katika ugavi wa fedha , serikali kuu hutenga fedha za basari kwa hazina ya ustawi wa maendeleo ya maeneo bunge CDF.
kila eneo bunge nchini hupokea zaidi ya shilingi milioni mia moja kutoka kwa serikali ya kitaifa kupitia hazina ya CDF , ili kufanikisha elimu kwa wanafunzi wasiojiweza.