WAZAZI POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUWAPELEKEA WANAO SHULE ZA CHEKECHEA.

Na Benson Aswani
Wazazi katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanao ambao wamefika umri wa kwenda shule wanahudhuria masomo katika shule za chekechea na kutokaa nao nyumbani.
Ni wito wake gavana wa kaunti hii John Lonyangapuo ambaye amesema kuwa serikali yake itaendelea kujizatiti kuhakikisha kuwa inatoa mazingira bora kwa wanafunzi hao hasa katika shule za chekechea kupitia kuweka vifaa hitajika kufanikisha masomo ya watoto katika shule hizo.
Aidha Lonyangapuoa amesema kuwa serikali yake itaendelea kuwekeza katika elimu hasa kupitia ujenzi wa madarasa katika shule za chekechea pamoja na kuwaajiri walimu zaidi lengo kuu likiwa kuhakikisha kuwa kile shule ina angalau walimu wawili.