WAZAZI MAENEO YA MIPAKANI WATAKIWA KUWAPELEKA WANAO SHULENI.
Wazazi hasa maeneo ya mipakani katika kaunti hii ya Pokot magharibi wametakiwa kuhakikisha kuwa wanao wanaripoti shuleni wakati huu ambapo shule zimefunguliwa kwa muhula wa kwanza.
Kulingana na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Holy cross Kacheliba Stanley Pilakan idadi ya wanafunzi ambao wamejitokeza katika shule nyingi maeneo hayo ni ya chini mno.
Amewataka wazazi kutohofu kutokana na kutokuwa na mahitaji yote kwa mwanafunzi kujiunga na kidato cha kwanza na badala yake kuzungumza na wakuu wa shule hizo ili kuweka mikakati ya kushughulikia mahitaji hayo baadaye wakati wanao wapo shuleni.
Aidha amewashauri wazazi katika maeneo ambako kumeshuhudiwa utovu wa usalama kuhakikisha wanao wanaripoti shuleni kutokana na hakikisho la serikali kuwa mikakati ya usalama imewekwa maeneo hayo.