WAZAZI KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALEMAVU

Na Dismas Terer
Wito umetolewa kwa wazazi walio na watoto wanaoishi na ulemavu kutowaficha watoto hao na badala yake kuwatoa ili waweze kupokea msaada unaostahili kielimu.
Akizungumza baada ya kuzinduliwa rasmi bweni na madarasa mawili katika shule ya walemavu ya Keringet ambao umefadhiliwa na hazina ya walemavu NFDK, afisa katika idara ya elimu kaunti hii ya Pokot magharibi Joshua Kosilei amesema kuwa serikali imetenga fedha za kutosha za kuhakikisha watoto hao wanapata msaada unaostahili.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwakilishi wa mwenyekiti wa hazina ya walemavu nchini Kristina Kenyatta ambaye aidha amesema kuwa hazina hiyo itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika kufanikisha juhudia za kuhakikisha watoto hao wanasaidika.
Uongozi wa shule hiyo ukiongozwa na mwalimu mkuu Jane Mricho umepongeza hatua hiyo wakiesema kuwa itakuwa ya manufaa makubwa ikizingatiwa wanafunzi hao wa kiume na wakike walilazimika kutumia bweni moja kutokana na uchache wa miundo mbinu.