WAZAZI KAUNTI YA ELGEYO MARAKWET WASHAURIWA KUWAHIMIZA WANAO KUPANDA MITI


Wito umetolewa kwa wazazi kote nchini kuwahimiza wanao kupanda miti ili kusaidia katika harakati za taifa za kuhifadhi mazingira na kuimarisha kiwango chake cha misitu.

Akiongea baada ya kuwaongoza watoto katika upanzi wa miti kwenye kaunti ya Elgeiyo Marakwet mhasisi wa shirika la kijamii la Sikika na Don’t Touch Viola Barsulai amesema kuwa iwapo watoto watahimizwa kupanda miti basi watakua na jukumu la kutunza mazingira siku zijazo.

Kwa upande mwingine Barsulai amewashauri wazazi kuwa karibu na wanao ili kuwalinda dhidi ya dhulma za kingono.

Kadhalika amewataka wazazi kuripoti kwa mamlaka husika visa vya dhulma kwa wanao ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.