WAZAZI ELGEYO MARAKWET WAHIMIZWA KUWATUNZAA WANAO DHIDI YA MAHUSIANO YA KIMAPENZI.
Mwakilishi wadi maalum katika bunge la kaunti ya Elgeyo Marakwet Moreen Masit amewahimiza wazazi kaunti hiyo kuwashauri wanao hasa wasichana dhidi ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi wakiwa wachanga.
Masit ametaja matumizi ya mitandao ya kijamii kwa wasichana wengi na ambao ni wanafunzi kama moja ya sababu zinazowafanya wengi wao kuingia katika mahusiano hayo.
Masit aidha amewahimiza wazazi kuhakikisha kwamba wanapata mahitaji ya kimsingi wanao wa kike ambao wamevunja ungo ili kuwaepusha kuomba msaada kwa wanaume ambao huenda wakawapachika mimba pindi watakapowasaidia.