WAZAZI BARINGO WATAKIWA KUKUMBATIA ELIMU YA MTOTO MSICHANA.


Wazazi katika kaunti ya Baringo wameshauriwa kukumbatia elimu ya mtoto msichana kwa kuhakikisha kwamba wanao wa kike wanaenda shuleni sawa na watoto wavulana.
Akiongea katika eneo la Chemolingot katika eneo bunge la Tiaty kamishna kaunti ya Tharaka nithi Beverly Opwora amesisitiza kwamba ni haki ya kila mtoto kupata elimu kwa mujibu wa katiba.
Aidha Opwora ameongeza kuwa jamii yoyote inayomwelimisha mtoto msichana hupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
Kauli yake imekaririwa na mshirikishi wa serikali eneo la magharibi ya nchi Esther Maina ambaye pia amewashauri wakazi kuasi utamaduni wa ukeketaji na kuwaoza wasichana mapema.