WAWANIAJI VITI MBALIMBALI KAUNTI YA TRANSNZOIA WAMESEMA WATAHAKIKISHA USALAMA UNADUMISHWA KAUNTI HIYO
Viongozi akina Mama Kaunti ya Trans Nzoia wameelezea Imani kuwa uchaguzi mkuu wa Agosti 9 utakuwa wa amani na huru kwa wawamiaji wote.
Akuhutubu baada ya kuidhinishwa kuwania kiti cha uwakilishi wa akina Mama Kaunti ya Trans Nzoia Kwa chama cha Jubilee Bi Susan Nelima amesema akina Mama wamepiga hutua kubwa katika uongozi wa taifa, akipongeza hatua ya Martha Karua kuteuliwa naibu rais Mteule wa Azimio la umoja akisema hii in hatua ya kuafikiwa kwa thuluthi mbili ya uwakilishi wa akina mama.
Wakati huo huo Bi Nelima amepongeza chama cha Jubilee kutokana na hatua yake ya kutoa nafasi nyingi za uwakilishi na uteuzi kwa akina Mama, akisema anamatumaini kuwa chama hicho chini ya Uongozi wa Rais Uhuru Kenyatta itatwaa nafasi nyingi ya uongozi kwenye uchaguzi mkuu ujao wa Agosti 9.