WAWAKILISHI WADI WAPYA KATIKA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WAPOKEA MAFUNZO


Bunge la kaunti hii ya Pokot magharibi linatarajiwa kurejelea vikao vyake hapo kesho jumatano vikao ambavyo vinatarajiwa kutumika kuapishwa waakilishi wadi pamoja na kumchagua spika wa bunge hilo.
Wakizungumza baada ya kukongamana katika bunge hilo kupokea mafunzo hasa kwa wanaoingia bungeni kwa mara ya kwanza, waakilishi wadi hao wameahidi kuhakikisha kuwa wanawahudumia vyema wakazi ikiwemo kuhakikisha kuwa serikali ya kaunti inawajibika inavyostahili.
Aidha waakilishi wadi wateule katika bunge hilo wametumia fursa hiyo kupongeza kupewa fursa hiyo na vyama mbali mbali kaunti hii wakiahidi pia kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwani pia wana jukumu kubwa la kutekeleza kwa wananchi.