WAWAKILISHI WADI WA POKOT MAGHARIBI WAPONGEZWA KWA KUPASISHA MSWADA WA MAREKEBISHO YA KATIBA WA 2020


Mbunge wa Pokot Kusini David Pkosing ameendelea kuwapongeza wawakilishi wadi katika kaunti ya Pokot Magharibi kufuatia hatua yao ya kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba ya mwaka elfu mbili ishirini.
Akiwalenga baadhi ya viongozi wanaopinga ripoti hiyo katika kaunti hii, Pkosing amewataka kujitokeza waziwazi badala ya kulisuta bunge la kaunti hii kwa kuipitisha ripoti yenyewe bila pingamizi.
Amesisitiza haja ya kupitishwa kwa mswada huo katika mabunge yote ya kaunti na ya kitaifa kutokana na manufaa yaliyoko katika ripoti hiyo.
Amesema kaunti hii itafaidika pakubwa kwa ugavi wa mapato ya asilimia thelathini na tano iwapo mswada huo utapitishwa katika kura ya maoni.