WAWAKILISHI WADI KUTOKA KAUNTI YA TRANS NZOIA WATAKA KINOTI KUSIMAMISHWA KAZI


Wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Trans Nzoia wamemrai rais Uhuru Kenyatta kumfuta kazi mkurugenzi wa idara ya upelelezi DCI George Kinoti kufuatia tangazo lake kwamba analenga kuendelea kufuatilia kesi za machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka wa alfu mbili na saba.
Mwakilishi wadi wa Kinyoro Lawrence Mokosu ambaye vilevile ni mwandani wa karibu wa naibu wa rais Wiliam Ruto amesema mara kadhaa Kinoti amekuwa akizungumzia maswala fulani bila kuwajali wananchi.
Hayo yanajiri huku rais Uhuru Kenyatta akimwonya vikali Kinoti kufuatia kauli hiyo.
Ikumbukwe kwamba Kinoti alisema alinukuliwa visivyo na kwamba matamshi yake hayakulenga kufufua kesi za awali ila kuchunguza madai ya vitisho vinavyotolewa na watu mbalimbali.