WAUZAJI WA VILEO KWENYE KAUNTI YA TRANS NZOIA WAMEPATA AFUENI YA SIKU 60 KUHUDUMU HUKU BUNGE LIKISAKA MWAFAKA WA UTOAJI LESENI.


Wauzaji wa vileo kwenye kaunti ya Trans Nzoia wamepata afueni baada ya bunge la kaunti kuwapa siku 60 ya kuhudumu ikisaka mwafaka wa utoaji leseni.
Kulingana na spika wa bunge hilo Joshua Werunga ni kwamba hatua ya kusitisha huduma za wafanyibiashara hao huenda ikawapa hasara zaidi ikizingatiwa kwamba biashara zao zilifungwa kutokana na janga la korona.
Wakati uo huo wito umetolewa kwa idara ya polisi na machifu kutowatia mbaroni wale ambao watakuwa wanahudhuria sherehe za kitamaduni na kunywa pombe aina ya busaa msimu huu wa krisimasi na mwaka mpya.
Akitoa wito huo, kiongozi wa wachache katika bunge la kaunti ya Trans Nzoia Emmanuel Waswa, amesema kuwa sheria zilizowekwa na wizara ya afya ili kuthibiti maambukizi ya virusi vya corona utazingatiwa kikamilifu kwenye hafla hizo.
Kwa upande wake mwakilishi maalum Philip Nyongesa amewarai wawakilishi wadi kwenye kaunti hiyo kupitisha mswada wa kuhalalisha ugemaji na unywaji wa pombe hiyo aina ya Busaa pindi tu watakapo rejelea vikao vyao bungeni.