WAUZAJI POMBE HARAMU TRANS NZOIA WAONYWA.


Idara ya uisaloama kaunti ya Trans nzoia kwa ushirikiano na kamati ya kutoa leseni kwa wauzaji wa vileo wameanzisha mikakati ya kukabiliana na watu wanaoingiza pombe haramu kutoka taifa jirani la Uganda.
Katika kikao na wanahabari mjini kitale kamishina wa kaunti hiyo Sam Ojwang amesema inafedhehesha kuona ongezeko la pombe haramu ambayo haijaidhinishwa na shirika la kuangazia ubora wa bidhaa nchini KEBS hali ambayo hunda ikahatarisha maisha ya wananchi.
Ojwang ameonya kuwa kamati ya kusimamia usalama kaunti hiyo itaimarisha oparesheni ya kuwanasa wanaoendeleza biashara hiyo haramu ikiwemo kuingiza nchini sukari ya magendo pamoja na bidhaa zingine.