WAUGUZI TRANS NZOIA WATAKA IDADI YAO KUONGEZWA

Serikali ya kaunti ya Trans-nzoia imetakiwa kuajiri wa uguzi zaidi ili kusaidia kukabiliana na magonjwa mbali mbali ikiwa ni pamoja na janga la covid 19 kwani kwa sasa serikali ya kaunti ina wauguzi 550 pekee.

Ni wito wake muunguzi mkuu katika kaunti hiyo Catherine Majimbo ambaye amesema idadi hiyo ya wauguzi ni ya chini ikilinganishwa na idadi inayohitajika kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO) ya wauguzi 83,0000 kwa wagonjwa 10,000, akisema kaunti ya trans-nzoia ina upungufu wa wauguzi 1,500.

Aidha Majimbo ametaka serikali ya kaunti kuwaandalia wauguzi hao mafunzo ya mara kwa mara haswa kuhusiana na magonjwa ya kuambukizana kama njia moja wapo ya kukabiliana na magongwa hayo.