WATUMISHI WA UMMA WASTAAFU WATAKA KUONGEZEWA MARUPURUPU.
Na Benson Aswani
Watumishi wa umma waliostaafu katika kaunti hii ya Pokot magharibi sasa wanaitaka serikali kuongeza kiwango cha marupurupu ya kustaafu wanayopokea kwa sasa kwa asilimia 3.5.
Wakiongozwa na katibu wa shirikisho la wafanyikazi waliostaafu, senior citizens welfare association of retired persons kaunti hii ya Pokot magharibi Nicholas Domokwang, wamesema kuwa shilingi alfu 5 wanazopokea sasa hazitoshelezi mahitaji yao.
Domokwang amesema kuwa licha ya juhudi zao kuandikia idara husika ikiwemo tume ya kutathmini mishahara ya wafanyikazi wa umma SRC pamoja na ile ya huduma za umma kuhusu swala hilo hamna hatua ambazo zimechukuliwa kufikia sasa.
Domokwang ametoa wito kwa viongozi wa kaunti hii akiwemo seneta Samwel Poghisio na mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto kushinikiza nyongeza ya fedha hizo kupitia mabunge yote mawili la kitaifa na lile la seneti ili kuihakikisha kuwa wanashughulikiwa.