WATUMISHI WA UMMA WASTAAFU WATAKA KUJUMUISHWA KATIKA SHUGHULI ZINAZOHUSU UMMA.

Na Benson Aswani
Watumishi wa umma waliostaafu katika kaunti hii ya Pokot magharibi wanaitaka serikali kutowatenga katika shughuli ya kuwahusisha wananchi katika maswala mbali mbali ambayo yanatekelezwa na serikali na ambayo yanahitaji maoni ya wananchi.
Wakiongozwa na katibu wa shirikisho la wafanyikazi waliostaafu, senior citizens welfare association of retired persons kaunti hii ya Pokot magharibi Nicholas Domokwang, wamesema kuwa wana utaalam wa kutosha katika maswala mbali mbali na mawazo yao yanaweza kuwa ya manufaa makubwa kwa taifa.
Wakati uo huo Domokwang amelalamikia kutotimizwa ahadi ya serikali kuwasaidia wastaafu hao katika kipindi hiki cha janga la corona ambapo awali waliahidiwa shilingi alfu mbili kila mwezi za kujikimu kufuatia athari za janga hilo.