WATU WENYE UMRI WA MIAKA 58 NA ZAIDI KUFANYWA KIPAUMBLE KATIKA SHUGHULI YA SERIKALI YA UTOAJI WA CHANJO DHIDI YA CORONA


Serikali kupitia wizara ya afya imewaruhusu watu wenye umri wa zaidi ya miaka 58 kuanza kuchanjwa . Hatua hiyo imeafikiwa baada ya data ya visa vya maambukizi kufichua kwamba asilimia sitini ya wagonjwa wanaofariki dunia kutokana na makali ya corona ni watu wenye umri huo.
Katika waraka iliyotiwa sahihi na mweneyekiti wa kamati ya utoaji wa chanjo ya covid 19 dr. Willis Akhwale , wizara ya afya imesema agizo hilo linaendana na mapendekezo ya afya dunia who na ya kamati ya kitaifa inayoshughulia maambukizi ya virusi vya corona.
Agizo hilo imewataka wanasiasa, viongozi wa kidini na wale wa kijamii wamehimizwa kwamba watakuwa wa kwanza kuchanjwa ilikuwapa wakenya imani ya kuchanjwa na kwamba chanjo hiyo ni slama.
Awali serikali iliwafanya wahudumu wa afya, maafisa wa usalama ,walimu na vilevile viongozi wa kidini kipaumbele katika awamu ya kwanza ya utoaji wa chanjo ya Astra Zeneca.