WATU WAWILI WAAGA DUNIA KUFUATIA UVAMIZI ENEO LA KABEN ELGEYO MARAKWET.
Watu wawili waliuwawa akiwemo mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika chuo kikuu cha laikipia kwa kupigwa risasi wengine wawili wakiuguza majeraha mabaya baada ya wavamizi wanaoaminika kutoka eneo la pokot kuvamia eneo la kaben kaunti ya elgeyo marakwet.
Afisa mkuu wa polisi wa kaunti ndogo ya marakwet mashariki clemet mbavu amedhibitisha kisa hicho kusema zaidi wavamizi miambili kutoka pokot magharibi na mashariki walivamia eneo la malisho na kutekeleza mauaji hayo kabla ya kuiba ngombe miambili na kumi.
Mkuu huyo aidha alisema kuwa kwa sasa maafisa wa polisi wamekita kambi katika eneo hilo kudhibiti hali huku wakiwataka jamii za marakwet kutolipiza kisasi.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya mshirikishi katika eneo la riftvalley George Natembeya kuzuru eneo hilo na jamii hiyo mbili kuahidi kukomesha uhasama ulioko miongoni mwao.