WATU WATATU WAULIWA TOT ELGEYO MARAKWET.
Watu watatu wameuliwa kwa kupigwa risasi kufuatia shambulio ambalo limetekelezwa na washukiwa wa wizi wa mifugo katika eneo la Kapkoros Tot katika kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Kulingana na ripoti ya idara ya polisi, wanafunzi wawili kutoka shule moja ya eneo hilo ni kati ya waliouliwa huku mifugo zaidi ya 400 wakiibwa.
Watu wengine watano wamejeruhiwa kufuatia uvamizi huo na wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya kimisheni ya Kapsowar na ile ya Moi ya mafunzo na rufaa mjini Eldoret.
Kuuliwa kwa watatu hao kunajiri wiki moja tu baada ya watu wengine idadi sawa na hiyo kuuliwa kwa kupigwa risasi kwenye kaunti hiyo.