WATU WATATU WAUA BARINGO KUSINI NA WAVAMIZI.
Wakazi wa eneo la Tandar Lamaiywe wadi ya Mochongoi Baringo kusini katika kaunti ya Baringo wanagali wanaishi kwa hofu kufuatia shambulizi lililotokea jana ambapo watu watatu wanahofia kufariki huku wengine wawili wakijeruhiwa vibaya.
Inaarifiwa tatu hao walimiminiwa risasi wakati walipokuwa wakichunga mifugo ambapo wengine sita hawajulikani walipo baada ya kutokea uvamizi huo.
Wakazi wa eneo hilo sasa wanaitaka serikali kuhakikisha usalama unaimarishea eneo hilo ili kukomesha mauaji ya kila mara ya wakazi wakati wahalifu hao wakiendelea kuendeleze shughuli zao katika misitu ya eneo la baringo kusini.
Hata hivyo kamishina wa kaunti ya Baringo Abdirizak Jaldesa ametoa ripoti pinzani na hali ya kuuliwa kwa watatu hao akisema kuwa ni watu watatu pekee ambao walijeruhiwa na wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja kaunti ya Likipia.