WATU WATANO WAULIWA NA WAVAMIZI MARAKWET MASHARIKI.
Polisi wameimarisha doria eneo la Marakwet mashariki katika kaunti ya Elgeyo marakwet baada ya wezi wa mifugo kuvamia eneo hilo jana na kuwaua watu watano kwa risasi huku wengine watatu wakiuguza majeraha mabaya.
Inaarifiwa kundi moja la wafugaji 150 kutoka eneo la Tiati kaunti ya Baringo liliwavamia wafugaji wa kaunti ndogo ya Marakwet mashariki mwendo wa saa sita unusu mchana wa jana katika eneo la Literi kiban.
Wavamizi hao wameripotiwa kuvuka mpaka na kuingia katika kaunti ya Elgeyo marakwet na kuvamia vijiji kadhaa wakitaka kuiba mifugo katika eneo la kiokaban kaunti ya Elgeyo marakwet kabla ya kuanza kukabiliana.
Kamanda wa polisi kaunti ya Elgeyo marakwet Patrick Lumumuba amesema mauaji hayo yametokea kufuatia ufyatulianaji risasi baina ya polisi, wanakijiji na wezi hao.
Hata hivyo amesema hali ya kawaida imeanza kurejea.
Watu waliojeruhiwa katika uvamizi huo wanatibiwa katika hospitali ya kimishonari ya Kapsowar Marakwet magharibi.
Uvamizi huo unajiri siku kadhaa tu baada ya waziri wa usalama wa ndani ya nchi Dkt Fred Matiangi kuzuru maeneo hayo wiki jana na kutoa muda wa siku saba kwa wakazi kurejesha silaha na kusitisha wizi wa mifugo la sivyo serikali ianzishe oparesheni ya kuwasaka