WATU WANAOWAPACHIKA MIMBA WASICHANA WENYE AKILI TAHIRA WAONYWA KULE KAKAMEGA


Viongozi wa jamii ya watu wanaoishi na changamoto za ulemavu kaunti ndogo ya Navakholo kule Kakamega wametoa onyo kali kwa wanaumme walio na hulka ya kuwapachika wasichana wenye akili tahira kisha kukwepa majukumu ya malezi kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Akizungumza kule Navakholo kupitia mwenyekiti wao Bathews Wechuli wanadai kuwa idadi kubwa ya wasichana hao hupachikwa mimba na wanaumme ambao hukwepa majukumu ya malezi wakisema kuwa sasa imefika wakati wao kukabiliana na mkono wa sheria.
Wakizungumza katika kikao kilichoandaliwa kwa madhumuni ya kuweka mikakati ya kuimarisha jamii ya walemavu, katibu mkuu wa jamii hiyo Nicholas Osendo amewahimiza wazazi kuwapeleka wanao wanaoishi na ulemavu shuleni ili kuwapa fursa ya kuwania nyadhifa za kazi kama watu wengine.