WATOTO WAKISIWA KULA NDIZI YENYE SUMU KAKAMEGA


Huzuni umetanda katika kijiji cha Imadala eneo bunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega baada ya mtoto mmoja mwenye umri wa miaka 14 kufariki huku wengine wanne wa kati ya miaka 8 na 12 wakilazwa katika hospitali ya Kakamega baada ya kula ndizi zinazodaiwa kuwekwa sumu.
Inaarifiwa watoto hao walikula ndizi hizo kabla ya kuanza kulalamikia maumivu ya tumbo huku wakitapika na kuendesha.
Familia ya watoto hao imekashifu vikali kisa hicho na kutaka kufanywa uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha hali hiyo.