WATOTO WA KIKE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI WASHAURIWA KUJITUNZA


Wito umetolewa kwa watoto wa kike kaunti hii ya Pokot Magharibi kujitunza na kutojihusisha na maswala ambayo yatawapelekea kupachikwa mimba za mapema na kuathiri masomo yao.
Ni wito ambao umetolewa na naibu chifu wa kata ya Mabayai eneo la Alale ambaye pia ameonya wanaohusika na kuwapachika mimba watoto wa kike na kuwaharibia maisha yao kuwa watakabiliwa kulingana na sheria.
Alikuwa akirejelea kisa ambapo mwanafunzi wa kidato cha pili eneo hilo la Mabayai alitoweka na kuolewa japo alitafutwa na kupatikana, ambapo aliyehusika na kutoweka mwanafunzi huyo anazuliwa na maafisa wa polisi.