WATEMBELEA WASICHANA WALIOKWEPA UKEKETAJI NA NDOA ZA MAPEMA ORTUM

POKOT MAGHARIBI

Kampuni ya nguvu za umeme KPLC tawi la bonde la ufa kwa ushirikiano na washikadau wengine pamoja na wahandisi wamewatembelea wanafunzi wa shule ya msingi ya wasichana ya Ortum walionusuriwa baada ya kudaiwa kukwepa ukeketaji na ndoa za mapema.
Wahikdau hao waliwakumbuka wasichana hao kwa kuwapa chakula cha krisimasi na bidhaa nyingine muhimu ikiwemo visodo pamoja na ushauri nasaha.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa KPLC kipkemboi kibias bonde la ufa wamewashauri wanafunzi hao kuweka bidii katika masomo yao na kuwa watu ambao wanakubalika katika jamii siku za usoni ikizingatiwa kwamba kaunty ya pokot zaidi ya wanafunzi alfu moja wamekeketwa huku wengine wakiozwa mapema.
Wakati uo huo wasichana hao ambao ni ishirini na wanane wamehimizwa kujihusisha katika maswala ya talanta mbalimbali na baada ya masomo kuweza kuchagua taalum nzuri katika maisha yao na kuondoa dhana kwamba hawawezi maishani.faith koome ni mmoja wa washikadau.
Huyu haa ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya wasichana ya Ortum akielezea changamoto ya shule hiyo