WATAKAOKOSA NAFASI KATIKA VYUO VIKUU WATAKIWA KUJIUNGA NA VYUO VYA KIUFUNDI


Wakuu wa shule katika kaunti ya Trans nzoia ambao shule zao zilitia fora katika mtihani wa KCSE wamewahimiza watahiniwa ambao watakosa nafasi za kujiunga na vyuo vikuu kutokata tamaa na badala yake kujiunga na vyuo vya kiufundi.
Wakiongozwa na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Makunga Moses Wabwire, wakuu hao wamesema kuwa vyuo vya kiufundi huwapa wanafunzi mafunzo ya taaluma mbali mbali zikiwemo biashara kujikimu kimaisha na kuchangia ukuaji wa uchumi nchini.
Ni matamshi ambayo yamesisitizwa na mwalimu mkuu wa shule ya upili ya wavulana ya Boma Isaac Makokha.