WATAHINIWA WOTE KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI NA MIPAKANI PA KAUNTI YA ELGEYO MARAKWET NA TURKANA WAMEHAKIKISHIWA USALAMA WAO WANAPOUFANYA MTIHANI WAO
Mtihani wa kitaifa kwa darasa la nane [K.C.P.E] unaingia leo siku ya pili baada ya kuanza rasmi hiyo jana huku usalama ukiwa umeimarishwa maeneo mbali mbali ya kaunti hii ya Pokot magharibi kuhakikisha mtihani huo unafanyika kwa njia salama.
Kamishina wa kaunti hii Apollo Okello amesema kuwa , maafisa wa usalama wametumwa katika maeneo hatari kwenye mipaka ya kaunti za Pokot Magharibi, Elgeyo Marakwet na Turkana ambako kumekuwa na tatizo la usalama akielezea imani ya kutoshuhudiwa changamoto zozote.
Okello aliwatakia watahiniwa heri njema akisema kuwa wametayarishwa vyema .
Kwa upande wake mkurugenzi wa elimu eneo bunge la Kapenguria Charles manyara amesema mikakati yote imewekwa
kuhakikisha watahiniwa wanapewa wakati mwafaka na kuwa usambazaji wa vifaa vya mtihani ulianza vyema bila matatizo.
Aidha manyara amesema takriban wanafunzi 4150 wanafanya mtihani huo wa KCPE katika shule 165 kwenye kaunti hii huku visa vya mimba za mapema vikiwa vimepungua.
Inaarifiwa kwamba mwanafunzi mmoja mtahiniwa anaukaulia mtihani wake katika hospitali ya sigor baada ya kujifungua hiyo jana.