WASOMI BARINGO WATAKA KUTAFUTWA SULUHU KUHUSU UTOVU WA USALAMA KAUNTI HIYO.


Wasomi katika wadi ya marigat kaunti ya Baringo wanaitaka serikali kuu kwa ushirikiano na viongozi kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo la utovu wa usalama kwenye baadhi ya maeneo ya eneo bunge la Baringo kusini.
Wakiongea baada ya kuandaa mkutano wa pamoja wasomi hao wamesema kuwa serikali ina wajibu wa kuwahakikishia wananchi wake wote usalama wao na wa mali yao.
Wasomi hao wameongeza kuwa japo wadi hiyo haishuhudii utovu wa usalama, mamia ya wakazi wa wadi ya mochongoi wanaishi kwenye wadi hiyo kama wakimbizi baada ya kutoroka makwao.
Kuhusu maswala ya kisiasa wasomi hao wametangaza kwamba wanamuunga mkono mbunge wa eneo hilo charles kamuren kuchaguliwa kwa muhula wa pili afisini wakisema kwamba ana rekodi nzuri ya utendajikazi.