WASOMI BARINGO WATAKA JAMII ZA WACHACHE KUJUMUISHWA KATIKA SERIKALI IJAYO.


Wasomi kutoka jamii za walio wachache nchini wamewasilisha memoranda iliyo na mapendekezo wanayotaka yaangaziwe na utawala wa chama cha UDA iwapo kitatwaa uongozi wa taifa hili katika uchaguzi wa tarehe 9 mwezi agosti.
Wakiongea kwenye hafla iliyoandaliwa mjini marigat katika kaunti ya baringo wamesema kuwa watu wa jamii za walio wachache wataunga mkono mrengo wa kisasa utakawahakikishia k wamba kwamba matakwa yao yatashughulikiwa.
Wasomi hao wamesema kuwa jamii za walio wachache zimetengwa na serikali zilizotanguliwa katika nyanja tofauti kama vile utoaji wa ajira, elimu bora, maswala ya afya, usambazaji wa maji na pia uwakilishi katika nyadhifa za kisiasa.
Miongoni mwa yale wanayopendekeza ni kuteuliwa mtu wa jamii za walio wachache kushikilia wadhifa uwakilishi wadi na ubunge kwenye kaunti sita ambazo jamii hizo zinapatikana, kutambuliwa rasmi kwa baadhi ya jamii kama vile segwer, kuteuliwa mmoja wao kushikilia wadhifa wa ubalozi, miongoni mwa mengine.