WASIWASI WAIBUKA KUHUSU USALAMA MPAKANI PA KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI NA UGANDA.


Viongozi katika kaunti jirani ya Uganda wameelezea wasiwasi kuhusu ongezeko la utovu wa usalama katika maeneo ya amudmat, Moroto pamoja na maeneo mengine yanayopakana na kaunti hii hali wanayosema huenda ikawa mbaya zaidi iwapo haitashughulikiwa.
Wakiongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa LC5 wilaya ya Amudat William Poatum wamedai kuwa hali hii imechangiwa pakubwa mizozo kuhusu lishe ya mifugo, maji pamoja na umasikini miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo.
Poatum amewalaumu wadau husika kutoka pande zote mbili, kaunti hii ya Pokot magharibi na taifa jirani la Uganda kwa kulaumiana kuhusu hali hiyo akisema si wakati wa kunyosheana kidole cha lawama bali kutafuta suluhu ya kudumu kwa tatizo husika.