WASIMAMIZI WA VIJIJI BUNGOMA WATAKA KULIPWA MISHAHARA


Wito umetolewa kwa serikali kuangazia kuanza kuwalipa wasimamizi wa vijiji wanaosema kuwa wamefanya kazi ya kujitolea kwa miaka mingi.
Wakiongozwa na mmoja wa wakuu wa vijiji hao Peter Marudi kutoka wadi ya west Nalondo katika kaunti ya Bungoma, wakuu hao wamesema kuwa wanapitia hali ngumu ya maisha kwa sasa na ni wakati serikali inapasa kutambua mchango wao kwa kuwalipa mishahara.
Wakuu hao wamesema kuwa wanafanya kazi katika mazingira hatari kwani wakati mwingi hulazimika kutekeleza kazi zao nyakati za usiku na ni jambo la kuvunja moyo kuwa hamna malipo yoyote wanayopata mwisho wa siku.