WASHUKIWA WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KAPENGURIA BAADA YA KUPATIKANA NA VILEO HUMU NCHINI KUTOKA NCHI JIRANI YA UGANDA

Kesi kuhusu ukwepaji wa kodi inayowahusu washukiwa wawili kaunti hii ya Pokot magharibi imetajwa katika mahakama ya kapenguria ambapo washukiwa walitakiwa kujibu mashitaka dhidi yao.
Geoffrey Torotich ambaye ni dereva na Martine Siwotoi mwenye bidhaa zilizofaa kulipiwa ushuru walikamatwa na kuzuiliwa na polisi kwa madai ya kuingiza vileo nchini kutoka taifa jirani la Uganda bila kufuata taratibu zinazostahili kisheria.
Kulingana na rekodi za mahakama, wawili hao waliokamatwa tarehe 20 mwezi februari mwaka huu katika barabara ya Chepareria kuelekea ortum walikuwa wakisafirisha chupa za pombe zilizofaa kulipiwa ushuru wa hadi shilingi alfu 194,883.
Lori lililokuwa limebeba bidhaa hizo lilikamatwa na maafisa wa KRA waliokuwa wakilishuku.