WASHUKIWA WA UVAMIZI WASHAMBULIA MATATU NA KUWAJERUHI WATU WATATU MJINI LODWAR.


Wasafiri wanaotumia barabara kuu ya kutoka lodwar kuelekea kitale wamejawa hofu na kusitishwa kwa usafiri baada ya matatu moja iliyokuwa ikitoka lodwar kuelekeamjini Kitale kaunti ya Trans nzoia kushambuliwa kwa kumiminiwa risasi.
Kulingana na joseph korir mkaazi wa lodwar aliyekuwa ndani ya gari lililoshambuliwa walimiminiwa risasi na wavamizi hao walipofika eneo la kws ambapo mmishonari mwanammke aliyekuwa katika gari hilo mvulana mdogo na dereva wa matatu hiyo walijeruhiwa.
Watatu hao walipokea huduma ya kwanza katika hospitali ya kainuk na kisha dereva akasafirishwa hadi eldoret katika hospitali ya mafunzo na rufaa kwa upasuaji wa kuondoa risasi iliokwama mguuni.
Kamanda wa polisi kaunti ya Turkana samwel ndanyi anasema maafisa wa usalama wanaendelea kuwasaka wahalifu hao.