WASHIKADAU KUTOKA KAUNTI YA TURKANA WAAHIDI KUHAKIKISHA VISA VYA MIMBA ZA MAPEMA ZINAPUNGUA
Mimba za mapema miongoni mwa wasichana na dhulma za jinsia ni baadhi ya changamoto zinazowakumba wasichana na wanawake katika kaunti ya turkana
Changamoto ambazo zimewaathiri wengi na sera zilizopo zikionekana kuwa pengo linalochangia visa hivyo
Hata hivyo serikali ya canada kwa ushirikiano na mashirika ya care international na adra zitatoa mafunzo kwa wasichana na wanawake katika kaunti nne zikiwemo kajiado, nairobi, siaya na turkana zinazoshuhudia visa hivyo kwa wingi
Stella waiguru ni afisa mkuu katika kitengo cha maswala ya kupanga uzazi katika wizara ya afya nchini
Kulingana na jane ejele ambaye ni waziri wa afya kaunti ya turkana, kaunti hiyo ni mojawapo ya kaunti zinazonakili visa vingi vya mimba za mapema na dhulma za kijinsia
Naye joyce olegiron mwanaharakati wa maswala ya jinsia anataja tamaa ya mali na kukosa masomo kama changamoto zinazochangia visa hivyo kaunti ya turkana