WASHIKA DAU KATIKA WIZARA YA MIPANGILIO YA SERIKALI WAZURU KAUNTI YA POKOT MAGHARIBI
Washikadau katika wizara ya mipangilio ya serikali hiyo jana wamezuru kaunti ya Pokot Magharibi kwa lengo la kuangazia na kuweka wazi ripoti inayohusu maswala ya kiuchumi, democrasia, maendeleo ya jamii sawa na utendakazi wa mashirika mbali mbali inayolenga kuimarisha uchumi wa mataifa ya bara la afrika.
Wakiongozwa na katibu katika wizara hiyo Saitoti Torome wanasema ripoti hiyo ina umuhimu mkubwa kwa taifa la Kenya kwani inangazia pakubwa mipango na mikakati inayokusudiwa na serikali kwa lengo la kukabili changamoto mbali mbali inayokumba taifa.
Aidha Torome anasema Kenya ni baadhi ya mataifa machache ambayo yana uhuru wa demokrasia kwani kila mwanachi ana uhuru wa kujieleza sawa na kumchagua kiongozi anayempenda mradi haikiuki sheria za nchi.
Wakati uo huo anasema tangu serikali za kaunti kugatuliwa na katiba ya mwaka 2010 kuanza kutumika matatizo mengi yaliyokuwa yakirudisha utenda kazi wa taifa hili nyuma yametatuliwa bila ugumu wowote.