WASAGAJI NAFAKA TRANS NZOIA WADINDA KUSHUSHA BEI YA UNGA.


Wasagaji nafaka mjini Kitale katika kaunti ya Trans nzoia wamesema kuwa hawatakubali kuuza unga wa mahindi pakiti kilo mbili kwa shilingi 100 hadi serikali itakapowafidia.
Wakiongozwa na Robert Wanyonyi, wasagaji nafaka hao wamesema kuwa kufikia sasa hamna mikakati ambayo imewekwa na serikali kuhusu jinsi watakavyofidiwa wakisema watakadiria hasa kubwa iwapo watauza unga kwa bei iliyotangazwa na serikali.
Hata hivyo msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amewahakikishia wasagaji nafaka na wauzaji wa unga wa mahindi kwamba watafidiwa, akiwaonya wale watakaokiuka agizo hilo kuwa huenda serikali ikalazimika kuwachukulia hatua.