WAPIGA KURA WATAKIWA KUJIFUNZA KWA MAKOSA YA UCHAGUZI MKUU ULIOPITA POKOT MAGHARIBI.


Wakazi wa kaunti hii ya pokot magharibi wametakiwa kuwa makini katika uchaguzi mkuu wa tarehe 9 mwezi agosti na kufanya uamuzi wa busara.
Akizungumza na kituo hiki naibu gavana Nicholas Atudonyang amewataka wakazi kujifunza kutokana na uchaguzi mkuu uliopita na kufanya maamuzi ambayo yatawapelekea kupata viongozi watakaohakikisha maendeleo yanaafikiwa ili kuimarisha uchumi wa kaunti hii.
Kuhusu mswada wa mabadiliko ya sheria za uchaguzi hasa katika upeperushaji wa matangazo ya matokeo ya kura, Atudonyang amesema wataunga tu mkono sheria ambazo zitahakikisha kunadumishwa uwazi na kutekelezwa haki ya mpiga kura katika kutangaza matokeo hayo.

[wp_radio_player]