WAPIGA KURA 220,026 WASAJILIWA POKOT MAGHARIBI


Afisa wa uchaguzi katika tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kaunti hii ya Pokot Magharibi Joyce Wamalwa amesema Jumla ya wapiga kura alfu 220,026 wamesajiliwa kuwa wapiga kura.
Katika mahojiano ya kipekee na kituo hiki Bi. Wamalwa aidha amesema kuwa vituo vya kupigia kura katika kaunti hii ni 857 pamoja na kimoja cha magereza ambacho kinafanya idadi ya jumla ya vituo hivyo kuwa 858.
Bi. Wamalwa amewataka wagombea wa nyadhifa mbali mbali kutumia wakati huu wa kampeni kuwahimiza wafuasi wao kuwa waangalifu na kutoharibu mali ya shule wakati watakaposhiriki uchaguzi mkuu wa mwezi agosti kwani vituo vingi vitakavyotumika katika shughuli hiyo ni shule.
Wakati uo huo ametumia fursa hiyo kuwaonya wagombea wa ugavana wa vyama vya UDA na KUP katika kaunti hii dhidi ya kwenda kinyume cha sheria za uchaguzi akionya huenda wakazuiwa kuwania viti hivo iwapo hawatawadhibiti wafuasi wao wanaohusika vurugu ikiwemo kuharibu mabango ya wagombea pinzani.